KISWAHILI
“Lakini kabla ya kompyuta kuwa kitu kisicho na uhai, na kabla ya Udhibiti wa Misheni haujatua Houston; kabla ya Sputnik ilibadilisha mwendo wa historia, na kabla ya NACA kuwa NASA; kabla ya kesi ya Mahakama ya Juu kuhusu Brown dhidi ya Bodi ya Elimu ya Topeka [jimbo la Kansas] ilithibitisha kwamba utengano haukuwa sawa, na kabla ya ushairi wa hotuba ya Martin Luther King Jr. "I Have a Dream" imevumisha mlio kwenye ngazi za Lincoln Memorial, Wanakompyuta wa West Langley [cheo cha kazi cha watu waliofanya kazi hii] walikuwa wakisaidia Marekani itawale angani, utafiti wa angani hiyo, na teknolojia ya kompyuta, wakijitengenezea mahali kama wanahisabati wanawake ambao pia walikuwa Weusi, wanahisabati Weusi ambao pia walikuwa wanawake.”
- Margot Lee Shetterly, katika dondoo kutoka kitabu chake Hidden Figures: The American Dream and the Untold Story of the Black Women Mathematicians Who Who Helped Win the Space Race (2016)
ENGLISH TRANSLATION
“But before a computer became an inanimate object, and before Mission Control landed in Houston; before Sputnik changed the course of history, and before the NACA became NASA; before the Supreme Court case Brown v. Board of Education of Topeka established that separate was in fact not equal, and before the poetry of Martin Luther King Jr.’s “I Have a Dream” speech rang out over the steps of the Lincoln Memorial, Langley’s West Computers [the job title of the people who did this work] were helping America dominate aeronautics, space research, and computer technology, carving out a place for themselves as female mathematicians who were also black, black mathematicians who were also female.”
- Margot Lee Shetterly, in an excerpt from her book Hidden Figures: The American Dream and the Untold Story of the Black Women Mathematicians Who Helped Win the Space Race (2016)
Kuhusu (About):
KISWAHILI
Margot Lee Shetterly ni mwandishi wa Marekani, mjasiriamali, na msafiri shupavu ambaye aliishi miaka 11 huko Mexico. Kwa sasa, yuko kwenye likizo refu ili akifanye kazi kwa kitabu kipya. Kitabu chake cha Hidden Figures kilitengenezwa kuwa filamu—trela hiyo iko hapa chini.
ENGLISH TRANSLATION
Margot Lee Shetterly is an American author, entrepreneur, and intrepid traveler who spent 11 years living in Mexico. She is currently on a writing sabbatical, working on a new book. Her Hidden Figures book was made into a movie—that trailer is below.
KISWAHILI: Asante na tutaonana tena,
Mmerikani
ENGLISH TRANSLATION: Thank you and may we see each other again,
Mmerikani
Chanzo (source): Shetterly, Margot Lee. Hidden Figures: The American Dream and the Untold Story of the Black Women Mathematicians Who Helped Win the Space Race. New York: HarperCollins, 2016, page xviii. Kindle edition.
//END