Kushambuliwa Kingono Siyo Lazima Kuseme Wewe ni Nani
Sexual assault doesn't have to define you
KISWAHILI
Des Linden anamhoji Kara Goucher—wakimbiaji wa mbio ndefu wa Marekani na wanadishi wote wawili—kuhusu kitabu kipya cha Kara The Longest Race: Inside the Secret World of Abuse, Doping, and Deception on Nike’s Elite Running Team (2023). Kitabu cha Kara kinafichua hadithi isiyofurahisha kuhusu kocha wake, Alberto Salazar, na jinsi Kara alivyoishinda. Kitabu chake pia kinaangazia kandarasi za mbio za kitaalamu [za masafa marefu.]
ENGLISH TRANSLATION
Des Linden interviews Kara Goucher—both American long-distance runners and authors—about Kara’s new book The Longest Race: Inside the Secret World of Abuse, Doping, and Deception on Nike's Elite Running Team (2023). Kara's book reveals an uncomfortable story about her coach, Alberto Salazar, and how she overcame it. Her book also sheds light on professional [long-distance] running contracts.
KISWAHILI
[Katika dondoo iliyo hapa chini, Des anamwuliza Kara ni nini muhimu kwa wengine kuchukua nao kutoka kwa hadithi yake juu ya kocha wake wa awali, Alberto Salazar, ambaye sasa ameondolewa rasmi kwenye mashindano kutokana na "mwenendo mpotovu kingono" na Kituo cha SafeSport cha Marekani:]
"Sijioni kama mhasiriwa...na kwa nguvu nilikaidi kuzungumza juu ya kile kilichotokea kwa miaka mingi kwa sababu sikutaka huruma yoyote...na [ningetaka] kusema tu kwamba mambo yanaweza kutokea kwako, lakini jambo hilo halisemi wewe ni nani…. Mimi ni mtu yule yule...kabla ujue kitu hiki kunihusu...na siyo lazima jambo hilo liseme wewe ni nani.
"Ni [kushambuliwa kingono hiku] siyo lazima kuiba kutoka kwako kitu cho chote katika maisha yako yaliyosonga mbele na...kuna mengi ya fedheha isiyo kawaida na aibu katika hali hizi na...mtu anayepaswa kusikia aibu ni mtu ambaye alifanya hivyo kwako—si wewe.
"Na una maisha yako yote ya kuendelea, na...kusonga mbele kutoka kwayo. Siyo lazima kiwe kitu kinachokufuatalia kwa maisha yako yote. Hiyo tu, nadhani, ni muhimu kwangu."
- Des Linden akimhoji Kara Goucher kwenye podikasti yao mpya Nobody Asked Us with Des & Kara. Des anamwuliza Kara juu ya kitabu kipya cha Kara, The Longest Race, kilichochapishwa hivi karibuni.
ENGLISH TRANSLATION
[In the below excerpt, Des asks Kara what is important for others to take away from her story with her previous coach, Alberto Salazar, who is now permanently ineligible due to "sexual misconduct" by the U.S. Center for SafeSport:]
"I don't see myself as a victim...and I really resisted talking about what happened to me for years because I didn't want any pity...and [I would like] just to say that things can happen to you, but it does not define you.... I am the same person...before you knew this about me...and it doesn't have to define you.
"It [sexual assault] doesn't have to rob you of anything in your life moving forward and...there's a lot of weird embarrassment and shame in these situations and...the person who should feed ashamed is the person that did it to you—not you.
"And you have your whole life to move on, and...move forward from it. It does not have to be something that follows you for the rest of your life. Just that, I guess, is important to me.”
- Des Linden interviewing Kara Goucher on their new podcast Nobody Asked Us with Des & Kara. Des asks Kara about her new book, The Longest Race, which was recently published.
KISWAHILI: Asante na tutaonana tena,
Mmerikani
ENGLISH TRANSLATION: Thank you and may we see each other again,
Mmerikani
Chanzo (source): Goucher, Kara and Des Linden. "7. Des Interviews Kara on The Longest Race." On Nobody Asked Us with Des & Kara. March 14, 2023. Audio (podcast), 58:00 minutes; above excerpt is from 55:42 to 56:40. Retrieved from Spotify:
.
//END