Tafsiri Haifanywi kwa Karatasi ya Kufuatilia
Edith Grossman (1936-2023): A translation is not made with tracing paper.
[Scroll down for the English]
KISWAHILI
"Ushikamanifu hakika ndio lengo letu kuu, lakini tafsiri haifanywi kwa karatasi ya kufuatilia. Ni kitendo cha fasiri yenye mchanganuo mahututi.
“Acha nisisitize jambo lililo dhahiri: Lugha hufuata njia za historia nyingi sana na za watu binafsi, na hakuna malugha mawili, pamoja na maongezeko yao yote ya mila na ya utamaduni, yanayopatana kikamilifu.
[Walakini,] hayo [YANAWEZA] [malugha] kuunganishwa kwa tafsiri, kama picha inaweza kuunganisha harakati na hali ya kutotenda….”
- Edith Grossman (1936-2023), mfasiri wa fasihi, mtetezi wa tafsiri, akizungumza juu ya jukumu la mfasiri.
ENGLISH TRANSLATION
“Fidelity is surely our highest aim, but a translation is not made with tracing paper. It is an act of critical interpretation.
“Let me insist on the obvious: Languages trail immense, individual histories behind them and no two languages, with all their accretions of tradition and culture, ever dovetail perfectly.
[However,] they [languages] [CAN] be linked by translation, as a photograph can link movement and stasis….”
- Edith Grossman (1936-2023), literary translator and translation advocate, speaking about the role of the translator.
Kuhusu (About):
KISWAHILI
Edith Grossman (1936-2023) alikuwa mfasiri mashuhuri wa fasihi wa waandishi muhimu wa lugha ya Kihispania na mtetezi wa tafsiri, akisisitiza watafsiri waweke majina yao pamoja na mwandishi asilia kwenye jalada. Alikumbusha kila mara tasnia ya uchapishaji na wasomaji kwamba tafsiri huwaruhusu wasomaji kupata uzoefu wa fasihi ya nchi na tamaduni zingine. Alijaribu kuinua jukumu muhimu la kutafsiri katika kitabu chake kilichochapishwa na Yale University Press, Why Translation Matters (2010).
ENGLISH TRANSLATION
Edith Grossman (1936-2023) was a renowned literary translator of famous Spanish-language authors and a translation advocate, insisting translators have their name on the cover with the original author. She continually reminded the publishing industry and readers that translations allow readers to experience the literature of other countries and cultures. She sought to elevate the critical role of translation in her book published by Yale University Press, Why Translation Matters (2010).
KISWAHILI: Asante na tutaonana tena,
Mmerikani
ENGLISH TRANSLATION: Thank you and may we see each other again,
Mmerikani
Chanzo (source): Grossman, Edith. “Narrative Transmutations.” January 23, 2007. PEN America. Accessed December 14, 2023. https://pen.org/narrative-transmutations.