Ted Gioia in Swahili: His 8 Best Techniques for Evaluating Character (#5 and #6 of 8 total)
Which trait irritates them and do they listen more than they speak
[Scroll down for the English]
KISWAHILI
8 Mbinu Bora za Ted Gioia Kutathmini Sifa ya Mtu Fulani (#5 and #6 of 8 total)
“Ninatakia mtu angeniambia mambo haya nilipokuwa mdogo. Sasa ninazitumia ninapohitaji kupata tathmini ya watu ambao siwafahamu vyema bila kukawia….
#5 Tambuza tabia ambayo inamkera mtu fulani sana—kwa sababu hii ndiyo tabia ambayo hawaipendi zaidi mwenyewe.
#6 Je, wanaweza kusikiliza?
“Wakati unapokutana na watu katika mazingira ya aina yoyote, kuanzia kitaaluma hadi kijamii, wanaweza kuchagua:
(1) kuzungumza,
(2) kusikiliza, au
(3) kutofanya lolote.
“Nina tumainifu zaidi katika kundi la 1 kuliko la 3, lakini kundi la 2 ndilo adimu zaidi—nimekutana na wasikilizaji wachache wazuri katika maisha yangu yote. Lakini ni baadhi ya watu wenye matokeo zaidi ambao nimewahi kukutana nao.
"Mara nyingi kuna mwelekeo dhidi ya kusikiliza kama sehemu ya ujuzi wa mtu--ndiyo sababu hautawahi kuuona kwenye wasifu. Nina hakika wengi wenu wanaamini hiyo inaonyesha ulegevu au uvivu au dosari nyingine ya tabia. Nadhani mwitikio huu ni matokeo ya kuainisha vibaya watu wanaofanya (3) pamoja na wale wanaofanya (2).
"Wasikilizaji wakuu wana ujuzi wa ajabu wa ufahamu na elekevu. Wanaweza kutathmini hali kwa usahihi mkubwa, na kutenda kwa njia zinazoongeza ufanisi wa kikundi. Hakuna shirika linaloweza kuwa nao kutosha, na ikiwa una mmoja wa wasikilizaji hawa wakuu kama rafiki au mfanyakazi mwenzako, hivi karibuni utagundua kuwa wao ni rasilimali muhimu sana.”
[Asante Ted for kwa kunipa ruhusa ya kutafsiri hii!]
ENGLISH TRANSLATION
Ted Gioia’s 8 Best Techniques for Evaluating Character (#5 of 8)
“I wish somebody had told me these things when I was younger. I now practice them when I need to get a fast assessment of people I don’t know well….
#5 Identify what irritates people the most in others—because this is probably the trait they dislike most in themselves.
#6 Can they listen?
“When you encounter people in any kind of setting, from professional to social, they can choose to (1) talk, (2) listen, or (3) do neither. I have far more confidence in group 1 than 3, but group 2 is the rarest—I’ve met few great listeners in my entire life. But they are some of the most effective individuals I’ve ever encountered.
“There’s often a bias against listening as part of someone’s skill set—that’s why you will never see it on a resume. I’m sure many of you believe it indicates passivity or laziness or some other character flaw. I think this reaction is a result of mistaking people who do (3) with those who do (2).
“Great listeners possess extraordinary skills of awareness and comprehension. They can assess situations with tremendous accuracy, and act in ways that maximize group effectiveness. No organization has enough of them, and if you have one of these great listeners as a friend or colleague, you soon learn that they are an invaluable resource.”
[Thank you, Ted, for the permission to translate this!]
KISWAHILI: Asante na tutaonana tena,
Mmerikani
ENGLISH TRANSLATION: Thank you and may we see each other again,
Mmerikani
Chanzo (source): Gioia, Ted. “My 8 Best Techniques for Evaluating Character.” The Honest Broker on Substack (January 18, 2023). Accessed March 20, 2024. https://www.honest-broker.com/p/my-8-best-techniques-for-evaluating (link now fixed).