Ted Gioia in Swahili: His 8 Best Techniques for Evaluating Character (#4 of 8)
"The two most revealing documents about me are my calendar and monthly budget."
[Scroll down for the English]
KISWAHILI
8 Mbinu Bora za Ted Gioia Kutathmini Sifa ya Mtu Fulani (#4 of 8)
“Ninatakia mtu angeniambia mambo haya nilipokuwa mdogo. Sasa ninazitumia ninapohitaji kupata tathmini ya watu ambao siwafahamu vyema bila kukawia….
Je, wanawekezaji rasilimali zao mbili muhimu zaidi kwa namna gani?
“Ninaandika makala na vitabu, lakini hati mbili zinazonifunulia zaidi ni kalenda yangu na bajeti kimwezi. Najua baadhi ya wabashiri wanataka kutazama kiganja cha mtu ili kusoma maisha yao ya ujao, lakini ningependelea kutazama jinsi wanavyotumia wakati na pesa. Hizo hufunua kile mtu anachohusu.
"Hiyo ni kweli kwangu na kwako, na kila mtu mwingine. Ni rahisi kusema jambo sahihi, lakini wakati na pesa ni za thamani zaidi kuliko maneno. Angalia kwa makini jinsi watu wanavyotumia rasilimali hizo mbili na utawaelewa kwa kina sana."
[Asante Ted for kwa kunipa ruhusa ya kutafsiri hii!]
ENGLISH TRANSLATION
Ted Gioia’s 8 Best Techniques for Evaluating Character (#4 of 8)
“I wish somebody had told me these things when I was younger. I now practice them when I need to get a fast assessment of people I don’t know well….
How do they invest their two most valuable resources?
“I write articles and books, but the two most revealing documents about me are my calendar and monthly budget. I know some fortune tellers want to look at a person’s palm to read their future, but I’d prefer to take a glimpse at how they spend time and money. Those reveal what a person is really all about.
“And that’s true for me and you, and everybody else. It’s so easy to say the right thing, but time and money are far more precious than words. Watch carefully how people allocate those two resources and you will understand them at a very deep level.”
[Thank you, Ted, for the permission to translate this!]
KISWAHILI: Asante na tutaonana tena,
Mmerikani
ENGLISH TRANSLATION: Thank you and may we see each other again,
Mmerikani
Chanzo (source): Gioia, Ted. “My 8 Best Techniques for Evaluating Character.” The Honest Broker on Substack (January 18, 2023). Accessed March 20, 2024. https://www.honest-broker.com/p/my-8-best-techniques-for-evaluating (link now fixed).
This is cause for self-reflection…